Benki ya Dunia yaipa Tanzania trilioni 4.9

0
22

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba, ameishukuru Benki ya Dunia kwa kuitengea Tanzania jumla ya dola za Marekani bilioni 2.1 [sawa na TZS trilioni 4.9] katika mzunguko wa 20 wa IDA (Julai 2022 – Juni 2025) kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotarajiwa kukuza uchumi wa nchi pamoja na kupunguza umasikini.

Dkt. Nchemba ametoa shukrani hizo wakati akizungumza na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia, anayesimamia nchi za Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, Victoria Kwakwa wakati wa Mikutano ya Mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), inayoendelea Mjini Washington DC, Marekani.

“Lengo ni kuipunguzia nchi yetu kukopa mikopo ya kibiashara ambayo ni ghali sana na inasababisha deni la taifa kuwa juu. Tunashukuru kwamba hilo nalo mmelipokea.” ameeleza.

Send this to a friend