Benki ya Dunia yaipongeza Tanzania kwa jitihada za kuimarisha upatikanaji wa umeme

0
37

Benki ya Dunia (WB) imeipongeza Tanzania kwa kuchaguliwa na kuwa miongoni mwa nchi nne barani Afrika zilizoingizwa katika mradi wa Benki ya Dunia wa ‘ASCENT’ ambao unalenga kuimarisha upatikanaji wa umeme kwa wananchi.

Amesema hayo Mkurugenzi wa Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika wa Benki ya Dunia, Wendy Hughe wakati wa mazungumzo na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Doto Biteko ambaye amesema suala la upatikanaji wa umeme nchini lina umuhimu kiuchumi, kisiasa na kijamii, hivyo Serikali inapata msukumo mkubwa wa kuhakikisha nchi inakuwa na umeme wa uhakika.

Pamoja na kuishukuru benki hiyo kwa kutoa fedha za kuendeleza miradi mbalimbali ya nishati ukiwemo mradi wa umeme wa Rusumo (MW 80) ambao dola za Marekani milioni 340 [TZS bilioni 851] zimetolewa, na mradi wa kuunganisha umeme kati ya Tanzania na Zambia uliotolewa TZS trilioni 1.13, Dkt. Biteko amesema Serikali itaendelea kutoa ushirikiano kwa benki hiyo kutokana na faida zinazotokana na ushirikiano uliopo.

Sababu za Tanzania kuilipa kampuni ya Canada fidia ya bilioni 76

Ameongeza kuwa, fedha zinazotolewa na wadau wa maendeleo ikiwemo Benki ya Dunia zitasimamiwa ipasavyo ili zitumike kwa malengo kusudiwa na hivyo kusukuma mbele sekta ya nishati ili kuwawezesha wananchi wote kuutumia umeme kwa shughuli za kijamii na kiuchumi.

Send this to a friend