Benki ya NCBA yaapa kusaidia ukuaji wa biashara za viwanda vidogo na vya kati Tanzania

0
35

Benki yaelezea namna itakavyokuwa mstari wa mbele kuleta uwezeshaji wa kiuchumi kupitia ujumusishwaji wa kifedha huku ikiwahamasisha wanaojituma kufikia malengo yao ya ukuaji.

Agosit 19, 2020. Benki ya NCBA yaapa kusaidia biashara za viwanda vidogo na vya kati ili kuchochea ukuaji wa kiuchumi.

Haya yalisemwa na Mkurugenzi Mkuu na Afisa Mkuu Mtendaji wa Benki ya NCBA Margaret Karume kwenye kusheherekea ujio wa Benki hio nchini, tukio likiambatana na uzinduzi wa Makao Makuu ya Ofisi ya NCBA na Tawi lao Kuu mtaa wa Ohio, Amani House jijini Dar es Salaam.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo, Margaret Karume alisema kuwa, malengo ya Benki ni kuhamasisha wanaojituma kwenye safari yao ya mafanikio na kuchochea ukuaji wa kiuchumi nchini na zaidi. ‘Kupitia uvumbuzi wetu unaomzingatia mteja na uwekezaji kwenye bidhaa za kidijitali za benki, tuko tayari kuharakisha ukuaji na maendeleo katika sekta muhimu za kiuchumi kama vile biashara za viwanda vidogo, vya kati, mashirika, miradi mikubwa ya miundombinu na sekta ya kilimo’.

Nasisitiza ya kuwa juhudi zetu zitakuwa za kidijitali, Benki ya NCBA itawaweka watu na wateja wetu katikati ya uvumbuzi. Tutatendelea kuvumbua na kutoa huduma za bora za Kifedha – na zenye viwango vya teknolojia ya juu zinazokubalika kimataifa na za kimapinduzi kama vile M-PAWA na huduma zingine za benki mtandao (online banking) ili kukidhi na kuvuka mahitaji ya wateja wetu’. Aliongezea.

Tukio hilo lilihudhuriwa na mgeni rasmi ambae ndie Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mheshimiwa Dokta Ashatu Kijaji ambae alisisitiza namna ambavyo Serikali ya awamu ya tano inajitahidi kujenga uchumi wa viwanda chini ya uongozi wenye dira wa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dokta John Joseph Pombe Magufuli. Juhudi ambazo zimejidhihirisha baada ya Tanzania kujumuishwa katika Nchi yenye kipato cha Kati kabla ya muda husika.

‘Nathubutu kusema ya kuwa, sekta ya Kibenki ni nguzo muhimu katika kusaidia utoaji wa mali za Kifedha na upatakinaji wa mikopo kwa viwanda vidogo na vya kati. Mikopo hii mara nyingi huwa inawekezwa katika uendeshaji wa biashara, upanuzi, faida na kuongeza thamani kwa kila alieshiriki katika upatikanaji wa mapato.
Hili linaenda sambamba na maono ya Serikali ya awamu ya tano chini ya Mhe Rais Dkt John Joseph Pombe Magufuli ambae pasipo kuchoka yupo mstari wa mbele kuhakikisha ya kuwa tunasonga mbele katika mafanikio makubwa na jumuishi kama Taifa lenye fursa sawa kwa wote.
Ili kudumisha juhudi hizi na kwenda mbali zaidi, ni lazima tuwe na sekta imara ya Kifedha itakayoendesha uchumi jumuishi wa Kifedha nchini kote na kutoa bidhaa na huduma muhimu zitakazoongeza ukuaji wa kiuchumi wakati Sekta ya Kilimo inaendelea kuwa muhimu sana katia uchumi wetu kwasababu inaajiri asilimia sabini ya watu nchini Tanzania ambayo ina athari chanya katika ukuaji wa Biashara za viwanda vidogo vidogo, vya kati pamoja na vyama vya ushirika. Hivyo basi, ukuaji katika sekta hii kupitia upatikanaji wa mikopo yenye riba nafuu, pembejeo, mafunzo ya kuwajengea uwezo na programu zingine zitakazoongeza ufahamu wa Kifedha kwa wakulima na wafanyabiashara ni muhimu sana’. alinukuliwa.

Waziri aliipongeza benki ya NCBA kwa kujitolea kwao kikamilifu ili kuisaidia Serikali katika jitihada zake za kudumisha sekta ya Kifedha. ‘Ninafarajika sana Benki ya NCBA kuchukua hatua Madhubuti hususan kwenye bidhaa kama M-PAWA inayotoa upatikanaji rahisi wa mikopo wa haraka na uwekaji akiba kupitia njia za simu ya mkononi, hivyo kuleta ujumusishwaji wa Kifedha, ukuaji wa biashara za viwanda vidogo na kati na kuwasaidia watanzania wote kwa ujumla’.

Muakilishi kutoka Benki Kuu ya Tanzania Meneja wa Usimamizi wa taasisi za Fedha, Bw Nassor Omar, ambae alikuwa miongoni mwa wageni waheshimiwa katika uzinduzi wa Benki ya NCBA aliisifu benki hio kwa werevu wao wa kuwa mstari wa mbele kuleta ujumusishwaji wa Kifedha kupitia uvumbuzi wa kidijitali ili kuhakikisha kila mtu anapata huduma za Kifedha kirahisi.

Bw Omar alisema, ‘Naomba kusisitiza ya kuwa, ukomavu wa mifumo ya Kibenki ni nguzo muhimu kwenye kujenga uchumi usiotetereka. Hivyo basi, ujio wa Benki ya NCBA ni moja kati ya ongezeko tosha la kuimarisha nafasi ya Tanzania kama nchi yenye kipato cha kati, sambamba na malengo ya Serikali ya awamu ya tano’.

Uzinduzi wa Benki ya NCBA Bank inafuatia idhini ya uunganaji iliyotolewa na Benki Kuu ya Tanzania na benki hio kuanza rasmi huduma zake mnamo tarehe 8 Julai mwaka huu. Ndani ya siku zijazo, Benki hii isheherekea uzinduzi wa huduma zake kwenye matawi ambayo yamekwishaanza kazi kwenye mikoa ya Mwanza, Arusha na Zanzibar.

MWISHO

Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana na:-

NCBA BANK TANZANIA LIMITED
Caroline Maajabu Mbaga
Head; Marketing, Communications & Citizenship
Email: caroline.mbaga@ncbagroup.com
Tel: +255 (22) 2295000 / DL: +255 768 987008

Send this to a friend