Beno Kakolanya atoroka kambini Singida FG ikiikabili Yanga

0
93

Klabu ya Singida Fountain Gate imesema inasikitishwa na kitendo cha kipa wao Beno Kakolanya kutoroka kambini wakati timu hiyo ikikabiliwa na mchezo muhimu dhidi ya Yanga uliochezwa leo jijini Mwanza.

Katika taarifa iliyotolewa Aprili 14, 2024 na uongozi wa Singida imesema inaendelea kufuatilia taarifa za mchezaji huyo na wengine ambao wataonekana kuihujumu timu hiyo katika michezo itakayochezwa.

“Kitendo hiki kinaleta maswali mengi, hasa ukizingatia kuwa Beno ni mchezaji mzoefu na mmoja wa wachezaji wa kutumainiwa wa timu ya taifa,” imeeleza taarifa.

Singida Fountain Gate imekutana na Yanga SC Aprili 14, 2024 katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza ambapo timu hiyo imeburuzwa mabao matatu bila.

Send this to a friend