Bernard Morisson, sikio la kufa

0
64

Klabu ya soka ya Simba imemsimamisha kwa muda mchezaji Benard Morrison hadi suala lake litakapopatiwa ufumbuzi.

Kwa mujibu wa taarifa ya Simba,  Morrison amekuwa na tabia ya kutoka kambini bila ruhusa kinyume na utaratibu.

Mara ya mwisho Morrison alitoka kambini na uongozi wa benchi la ufundi ulilmpa maelekezo kuwa asirejee kambini hapo mpaka atakapoonana na Mtendaji Mkuu wa klabu ya Simba, Barbara Gonzalez.

Hata hivyo Morrison hakutii maagizo hayo hivyo kuendelea kukaa nje ya kambi.

“Kufuatia kadhia hiyo, uongozi wa klabu umemsimamisha kwa muda na kumtaka atoe maelezo ya maandishi kwa mtendaji mkuu wa klabu  ya Simba, na akishindwa hatua zaidi za kinidhamu zitachukuliwa,” imeeleza taarifa hiyo.

Morrison alisajiliwa na klabu ya Simba baada ya kuvunja mkataba na klabu ya Yanga kisha kufikishwa kwenye kamati ya nidhamu na wakati kesi yake ikiendelea, alisaini mkataba wake na klabu ya Simba  na baadaye kamati ya Sheria na Hadhi ya wachezaji ilibaini kuwa mkataba wake na Yanga ulikuwa na mapungufu hivyo ikamtangaza kuwa mchezaji huru.