BIASHARA ZITAENDAJE ENDAPO INTERNET ITAZIMIKA – XTOK

0
33

Tangu kuingia kwa Internet Tanzania na Dunia nzima, Biashara nyingi zimepata namna ya kujitangaza kwa kufikia wateja wao kwa urahisi, pia biashara mpya zimejitokeza kama wauzaji wa bidhaa mbali mbali wasio na maduka bali huuza kupitia njia ya mtandao. Kampuni za simu, Kampuni za mawasiliano, Bloggers ni moja ya mifano ya kampuni zilizofaidika kutokana na Internet.

Kwa upande mwingine kuna kampuni zilizo pitia kipindi kigumu kutokana na mabadiliko ya teknolojia kama magazeti, kampuni za matangazo ya mabango na nyingine nyingi.

Infinix Mobile Tanzania Kupitia XTOK – EVENT wameandaa mjadala mfupi kuhusu mada hii, “WHAT IS THE FUTURE OF BUSINESS IF THE INTERNET BECOMES OBSOLETE?” 

Mjadala Huu utaendeshwa siku ya Jumamosi, tarehe 7 ya mwezi Disemba katika ofisi za Sahara Ventures zilizopo barabara ya Bagamoyo Rd, Jengo la Bayport ghorofa ya 6, kuanzia saa 4 na nusu asubuhi mpaka saa 8 mchana. Ili kujiunga na mjadala huu unaweza jisajili  Hapa

Kutakuwa na wageni maalum ambao ni Mtaalamu wa Mawasiliano Princel H Glorious, Founder wa Ona Stories. Ndugu Cynthia Bavo ambaye ni C.E.O na Founder wa MyJobPass na Ndugu Anthony Luvanda ambaye ni Mjasiriamali/Public Speaker.

(Kuhusu XTOK)

XTOK ni event ambayo huandaliwa na kampuni ya simu, Infinix Mobile Tanzania kwa lengo la kuwakutanisha vijana wapenda teknolojia, ubunifu na trends mbali mbali ili kujadiliana kwa lengo la kutafuta suluhisho. Hii ni imara ya 5 kufanyika kwa event hii.

Send this to a friend