Bibi Harusi akamatwa kwa kuwalisha wageni bangi

0
48

Polisi wamemkamata bibi harusi, Danya Svoboda na mhudumu wake baada ya kubaini kuwa waliweka bangi kwenye chakula ambacho kilitolewa kwa wageni kweye harusi iliyofanyika Februari 19 katika jiji la Longwood, Florida.

Kukamatwa kwao kulitokea baada ya maafisa wa Polisi kuitwa kwenye sherehe ya harusi hiyo kusaidia wageni ambao walisema walihisi kana kwamba walikuwa wamepewa dawa za kulevya na baadhi kupoteza fahamu.

Hata hivyo vipimo vya chakula na vinywaji vilionekana kuwa na chembechembe za bangi.

Bibi harusi na mhudumu, Joycelyn Bryan wanakabiliwa na mashtaka ya kulisha watu bangi bila ridhaa yao.

Mmoja wa wageni waliohudhuria sherehe hiyo amesema alianza kuhisi tofauti baada ya kula, akiona kama amelewa.

Bangi kwa ajili ya matibabu ni halali huko Florida, lakini haijahalalishwa kwa ajili ya burudani tofauti na baadhi ya majimbo mengine Marekani.

Send this to a friend