Bibi wa miaka 78 akamatwa kwa kupora pesa benki

0
46

Polisi katika jimbo la Missouri nchini Marekani wanamshikilia bibi wa miaka 78 kwa tuhuma za wizi katika moja ya benki nchini humo.

Bonnie Gooch anadaiwa kuingia katika Benki ya Goppert akiwa amevalia barakoa nyeusi, miwani na glovu za plastiki na kukabidhi barua kwa mtoa pesa iliyosema “ninahitaji noti za thamani ya dola 13,000 (sawa na TZS milioni 30)”, huku akiamrisha kupewa pesa haraka.

Baada ya uporaji huo, Bi. Gooch aliacha barua inayosema “Asante samahani sikukusudia kukutisha” kabla ya kuondoka na pesa taslimu.

Baba atuhumiwa kumlawiti mtoto wake wa mwaka mmoja 

Waendesha mashtaka wamesema Maafisa wa Idara ya Polisi walimpata Bi Gooch kwenye gari lake akiwa ananuka pombe kali, huku pesa zikiwa zimetapakaa sakafuni.

Polisi wamedai Bi Gooch hakuwa na maradhi yoyote yaliyobainika, lakini kutokana na umri wake, idara hiyo inajaribu kuchunguza ikiwa kuna sababu zozote za kiafya zinazoweza kuchangia tukio hilo.

Hata hivyo si mara ya kwanza kwa Bi Gooch kukumbana na sheria, kwani inasemekana kuwa amewahi kukutwa na hatia mbili za wizi wa benki zamani, moja ikiwa huko California mnamo mwaka 1977 na nyingine mnamo mwaka 2020.

Hivi sasa, Bi Gooch yuko jela na anahitaji dhamana ya kiasi cha TZS milioni 58.

Send this to a friend