Bien: Mahusiano kwenye miaka ya ishirini ni kupoteza muda

0
57

Mwimbaji mkuu wa kundi la Sauti Sol nchini Kenya, Bien-Aime Baraza amesema hashauri watu waliopo katika umri wa miaka ya ishirini kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi kwani ni kupotezeana muda.

Bien amesema watu walio katika umri huo wanapaswa kujijali wenyewe na kusafiri kwa kuwa mtu aliyeko katika umri huo bado anajitafuta ajue kitu gani hasa anakihitaji.

Diamond aeleza sababu ya kuchukua 60% ya mapato ya wasanii WCB

“Siwezi kumpa ushauri mtu mwenye umri wa miaka ishirini awe kwenye mahusiano, ni kupoteza muda, angalau fanya kazi, usafiri, pia uwe na watu wengine huku na huko.”

Ameongeza kuwa, mtu akiwa katika umri huo “hajitambui, na mtu uliye naye pia hajitambui, unadhani unafanya nini? Mnajaribu kusuluhisha mambo pamoja, lakini mwisho wa siku, yaani, nadhani ni bora kuwa peke yako ikiwa uko katika miaka ya 20,” amesisitiza Bien.

Send this to a friend