Biharamulo: Walimu 6 watuhumiwa kujihusisha na biashara ya kuwauza wanafunzi kingono

0
54

Baadhi ya madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera wameomba kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa walimu sita wa Shule ya Sekondari ya Nyankatala wakiwatuhumu kuwashawishi wanafunzi wa kike kujiingiza katika biashara ya ngono.

Madiwani hao wamedai hali hiyo inasababisha kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa wanafunzi kwenye shule hiyo na kuomba hatua za haraka zichukuliwe.

Ombi hilo limetolewa kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo wakati wakijadili hoja mbalimbali ambapo wameeleza kuwa wanashangazwa kuona hatua hazichukuliwi licha ya kuundwa kwa Tume ya Awali ya Uchaguzi.

VETA yabuni miwani ya kumzuia dereva kusinzia

“Hawa wahusika ambao wamebainiwa katika vitendo hivi vya kuuza watoto wa kike kwa hamasa ya kuwaharibia masomo yao, kama tutakuwa tunakwenda kwa spidi ya taratibu hii je, kipindi hiki wakati tupo kwenye utaratibu wa kujiridhisha kuchukua hatua, watoto hawa wana uhakika upi wa kuwa salama?” amehoji mmoja wa madiwani.

Send this to a friend