Bilioni 100 za Rais kila mwezi kwenye mafuta ni neema kwa Watanzania

0
17

 

Na John Mwakanga, Mbeya

Kupanda kwa bei za mafuta ni janga linaloendelea kuitikisa Dunia kwa ujumla. Kwa kuelewa uzito wake kwa wananchi wa Tanzania, Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imejitwika jukumu la kupunguza gharama kwa wananchi kwa kutoa ruzuku ya bilioni 100 kila mwezi.

Juni 10, akiwa kwenye ziara ya kikazi Kagera, Rais Samia alitangaza kuwa serikali itatoa ruzuku ya shilingi bilioni 100 endelevu hadi hapo hali itakapokaa sawa.Uamuzi utakaomnufaisha kila Mtanzania moja kwa moja, sio tu wale wanaotumia vifaa vya moto kama magari na pikipiki bali kila mtu hata yule mjasiriamali mdogo.

Uamuzi wa Rais Samia kutoa bilioni 100 kila mwezi utashusha gharama za uzalishaji. Ikumbukwe kuwa baada ya mafuta kupanda bei (peroli, dizeli na mafuta ya kupikia), nauli na bidhaa mbalimbali za vyakula nazo zilipanda bei. Ni kwasababu mitambo inayotumika kwaajili ya uzalishaji wa bidhaa hizo hutumia pia mafuta.

Gharama za usafirishaji wa bidhaa pia zinaenda kupungua hivyo mtumiaji kununua bidhaa kwa bei ya afueni kwa ruzuku hiyo iliyotolewa na serikali ya awamu ya sita. Huku wawekezaji nao wakitumia fursa hiyo kuwekeza Tanzania kwani mwekezaji huangalia zaidi kupata faida kubwa kwa kuwa na changamoto chache.

Lengo la Rais Samia Suluhu Hassan kuchukua uamuzi huo wakati bado soko la mafuta duniani kote bado linatetereka ni kusaidia kuzuia bei ya mafuta isiendelee kwenda juu. Walau ibaki vilevile au ishuke ili mwananchi asiumie kwa hilo.

Ruzuku ni kiasi cha pesa ambacho hutolewa na serikali kwaajili ya kusaidia kupunguza gharama za uendeshaji au bidhaa kwa mtumiaji wa mwisho.

Send this to a friend