Bilioni 19.7 kukarabati Uwanja wa Uhuru

0
68

Serikali kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imesema Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) utasimamia ukarabati wa Uwanja wa Uhuru mkoani Dar es Salaam ambao utafanywa na kwa gharama ya shilingi bilioni 19.7.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa wakati wa utiaji saini wa mkataba huo ambao utachukua takribani mwaka mmoja, ukijumuisha ukarabati wa miundombinu ya eneo la kuchezea (pitch), eneo la kukaa watu, mifumo ya maji safi na maji taka, viyoyozi, sauti pamoja na kubadili milango na madirisha.

Kaimu Mkurugenzi wa Ushauri wa TBA, Arch. Victor Balthazar amesema timu ya wataalamu kutoka TBA imejipanga kuhakikisha inasimamia ukarabati wote utakaokwenda kufanyika sambamba na kuzingatia mapendekezo yaliyotolewa na Serikali juu ya kuongeza idadi ya watu kufikia elfu thelathini.

Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) uliingia Mkataba na Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo Februari 2023 kwa ajili ya kusimamia ukarabati wa viwanja saba nchini vikiwepo viwanja vya Uhuru na Benjamini Mkapa.

Send this to a friend