Binti (13) amuua mama yake kisa kumnyang’anya simu yake

0
49

Polisi nchini Kenya wanamshikilia msichana wa miaka 13 kwa tuhuma za kumuua mama yake mzazi kwa kutumia panga baada ya kutokea mvutano uliosababishwa na matumizi mengi ya simu.

Kulingana na mkuu wa polisi wa kaunti ndogo ya Transmara Mashariki, Boniface Kavoo, mama wa binti huyo mwenye umri wa miaka 55 alitaka kumpokonya simu binti yake baada ya kutofurahishwa na tabia ya binti huyo kuchati na kuzungumza na simu muda mwingi.

“Ni mazingira ambayo mama yake alitaka kumpokonya simu binti yake aliyokuwa akichati naye, inaonekana marehemu alikuwa mama mkali, na hakufurahishwa na msichana wake kufanya mawasiliano mengi bila yeye kujua,” ameeleza Kamanda Kavoo.

Mkenya aajiriwa kwenye nafasi za juu za mashirika 8 ya umma

Baada ya mvutano huo, katika hali ya kushanga mshukiwa aliokota panga na kumvamia mama yake kisha kumkata kichwani na ndipo alipofariki dunia baada ya kuvuja damu nyingi.

Baada ya mauaji, mshukiwa huyo anasemekana kutupa silaha ya mauaji kwenye choo cha shimo ili kuficha ushahidi lakini baadaye alikiri kumuua mama yake kwa kutompa uhuru wake.

Send this to a friend