Binti adaiwa kumchinja mama yake akimtuhumu kumuua mtoto wake

0
37

Watu wawili wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Geita kwa tuhuma ya kumuua kwa kumchinja mwanamke mmoja aliyetambulika kwa jina la Butamo Igonzele (70) mkazi wa kijiji cha Bumegezi wilaya ya Geita.

Jeshi hilo linawashikilia Joyce Julius ambaye ni mtoto wa marehemu na Juma Charles ambaye ni mkwe wa marehemu ambao inadaiwa walikuwa wanamtuhumu marehemu kuhusika na kifo cha mtoto wao ambaye alifariki wiki moja iliyopita.

Kigoma: Wanafunzi wanne waliozama mtoni wakienda shule asubuhi hawajapatikana

Tukio hilo limetokea Februari 23, 2023 usiku ambapo Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita, Kamishna Msaidizi wa Polisi Berthaneema Mlay amesema watu hao wanashikiliwa kwa ajili ya upelelezi zaidi.

Amesema watuhumiwa hao wamemakatwa baada ya uchunguzi wa awali kuonesha wanaweza kuhusika katika mauaji hayo.

Send this to a friend