Binti akamatwa kwa kuajiri mtu amuue mpenzi wake wa zamani

0
3

Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 26, Jaclyn Diiorio, anakabiliwa na mashtaka mazito baada ya kudaiwa kupanga njama ya kumuua mpenzi wake wa zamani, ambaye ni askari wa Polisi wa Jiji la Philadelphia mwenye umri wa miaka 57, pamoja na binti yake wa miaka 19.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, Diiorio alikutana na mtu kupitia programu ya kutafuta wapenzi ya Tinder, ambaye mtu huyo alikuwa akitoa taarifa kwa siri kwa polisi. Diiorio alidaiwa kuwasiliana naye kupitia simu na ujumbe mfupi kabla ya kukutana ana kwa ana, ambapo alieleza dhamira yake ya kutaka familia hiyo mbili kuuawa.

Ripoti zinaeleza kuwa Diiorio aliahidi kulipa dola 12,000 [TZS milioni 32,2] kwa mauaji hayo na tayari alikuwa amelipa kiasi cha awali cha dola 500 kabla ya kutiwa mbaroni wiki iliyopita huko Gloucester Township.

Wakati wa kukamatwa, Diiorio alikuwa na chupa ya dawa isiyo na lebo, ambayo ilisemekana kuwa na dawa aina ya alprazolam, dawa ya kutuliza wasiwasi na mshtuko isiyoruhusiwa kisheria.

Diiorio amefunguliwa mashtaka mawili ya jaribio la mauaji ya daraja la kwanza, shtaka moja la kula njama ya kuua, na shtaka moja la kumiliki dawa hatari isivyo halali.

Send this to a friend