Binti akamatwa na kadi 23 za benki, Polisi waeleza alivyozitumia kuiba
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia Bi Halima Juma (23) mkazi wa Chalinze kwa tuhuma za wizi wa fedha kwenye mashine za kutolea fedha (ATM)
Mnamo tarehe 19/11/2019 katika benki ya CRDB tawi la Mbagala akiwa katika ATM hizo, aidha alimtilia mashaka binti huyo aliyekuwa kwenye chumba cha ATM ya benki hiyo akijifanya kuwasaidia wazee na wastaafu wasiojua kutumia ATM mashine vizuri, lakini lengo lake ni kuchukua namba za siri za wastaafu na wazee hao na kisha kuwabadilishia ATM kadi zao na baadaye kuwaibia fedha kwenye akaunti zao kwa kutumia kadi halisi za wahusika baada ya kuwabadilishia kadi na kuchukua namba za siri.
Mtuhumiwa huyo alikamatwa na askari wanaolinda Benki hiyo na alipopekuliwa alikutwa na ATM kadi 23 za watu mbalimbali za benki tofauti tofauti zikiwa katika pochi yake huku akiwa amezificha katika sehemu zake za siri ukeni.
Kadi hizo ni kama ifuatavyo;
1.CRDB kadi 07
2.NMB kadi 06
3.NBC kadi 02
4.AMANA kadi 02
5.POSTA BENKI kadi 02
6.ACB kadi 01
7.STANIBIC kadi 01
8.DTB kadi 01
9.EQUITY kadi 01
Mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa na atafikishwa mahakamani hivi karibuni.