Binti amshtaki ‘baba mkwe’ kwa kukataa asiolewe na kijana wake

0
46

Binti mmoja katika jimbo la Kaduna nchini Nigeria amemshtaki baba mkwe wake katika Mahakama ya Kiislamu (Sharia) kwa kumzuia kuolewa na mpenzi wake, Bashir Yusuf.

Kwa mjibu wa jarida la The Daily Trust, Halima Yunus (ambaye ni mlalamikaji) aliiambia mahakama kuwa amependana Yusuf, lakini baba yake Yusuf amekataa asimuoe.

Aidha, baba yake Halima, Ibrahim aliiambia mahakama kwamba alikuwa anafahamu kuhusu mapenzi baina ya binti yake na Yusuf, lakini alikuwa hajatimiza vigezo vya kuoa.

Amedai zaidi kuwa alimtuma mchumba wa binti yake awalete wazazi wake lakini hakurudi tena kwa takribani mwaka mmoja.

Send this to a friend