Biskuti yamponza dereva bodaboda

0
53

 

Ivan Cheyo (18), dereva wa bodaboda mkazi wa Vwawa wilayani Mbozi mkoani Songwe, amejikuta akiwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa baada ya kula biskuti zinazosemekana zenye madawa ya kulevya.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Janneth Magomi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa, dereva huyo alikodiwa na watu wasiojulikana katika kijiwe chake na kesho yake asubuhi Aprili 20 alionwa na wanfunzi waliokuwa wakienda shule akiwa hajitambui.

“Dereva huyu wa bodaboda anaendelea kupata matibabu Hospitali ya Rufaa, maana alikutwa amelala kwa kutelekezwa na wezi hao kando ya mto akiwa hajitambui,” ameeleza.

Ivan alipata mkasa huo Aprili 19 mwaka huu, saa 10 jioni baada ya kukodiwa na wanaume wawili na kuwapeleka katika Kijiji cha Haraka, kata ya Hezya Mbozi.

Akizungumza kwa shida baada ya kurejewa na kumbukumbu zake Ivan alisema, wakiwa safarini walisimama katika kijiji cha Manyara na wateja wake kununua soda na biskuti na ndipo mmoja wa wanaume hao alimpa biskuti na baada muda alianza kuishiwa nguvu na kujikuta hospitalini.

Send this to a friend