Biteko aiagiza REA kuachana na wakandarasi wazembe

0
40

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt Dotto Biteko ameuagiza Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kufanya tathmini ya wakandarasi wanaotekeleza miradi ya umeme na kuachana na wale wanaoshindwa kuendana na kasi ili ifikapo Juni 2024, miradi yote nchini iwe imekamilika.

Akizungumza kutoka wilaya ya Mtwara mkoani Mtwara wakati akiwasha umeme katika vijiji vya Nachenjele na Naliendele katika ziara yake ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo amesema serikali imetoa TZS bilioni 170 kwa ajili ya utelekezaji wa miradi ya REA mkoani Mtwara.

“REA msicheke na wakandarasi wanaokwamisha utelekezaji wa malengo yetu na hili linahitaji usimamizi wa karibu kwa kila miradi” amesema Dkt Biteko huku akisisitiza kuwa “tunataka tutoke kwenye miradi ya vijiji na tuingie katika kampeni ya kitongoji kwa kitongoji baada ya uchaguzi mkuu ujao.”

Dkt. Biteko ‘awatumbua’ mameneja wa TPDC na TANESCO

Aidha, Dkt Biteko ameitaka REA na TANESCO kutumia vifaa vya usambazaji umeme vinavyozalishwa na viwanda vya ndani badala ya kuagiza nje ya nchi.

Send this to a friend