Bodaboda jela miaka 30 kwa kumbaka abiria wake mkoani Kigoma

0
60

Mahakama ya Hakimu Mkazi Uvinza imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela dereva wa bodaboda, Ruben Gerishon (24) mkazi wa Kijiji cha Mlela wilayani humo mkoani Kigoma baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka abiria wake.

Sambamba na hukumu hiyo, mahakama imetaifisha pikipiki iliyokuwa ikitumiwa na mshitakiwa huyo yenye namba za usajiili MC 601 DLB na sasa ni mali ya serikali.

Mwendesha mashitaka wa polisi aliieleza mahakama kwamba Septemba 7 mwaka jana, mshitakiwa huyo alikodiwa na msichana mwenye miaka 24 ampeleke Kijiji cha Kidahwe, baada ya kukosa usafiri katika eneo hilo, na ndipo mwanaume huyo alipotekeleza ukatili huo walipokuwa njiani.

Akitoa hukumu ya kesi hiyo Hakimu Mkazi Misana Majura aliiambia mahakama kwamba amejiridhisha kulingana na ushahidi ulitolewa mahakamani hapo ambao umethibitisha kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo.

Send this to a friend