Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imeongeza idadi ya wachezaji wa kigeni wanaoweza kusajiliwa na vilabu nchini pamoja na idadi ya wachezaji hao ambao wanaweza kushiriki katika mchezo mmoja.
Katika taarifa yake, TPLB imesema kuwa kanuni mpya ambazo zimeanza kutumika zinaruhusu klabu kusajili wachezaji wasiozidi 12 na kuwatumia wachezaji wote katika mchezo mmoja.
Tanzania na Uganda kuandaa AFCON 2027
Kabla ya maboresho hayo, klabu zilikuwa zinaruhusiwa kusajili wachezaji wa kigeni wasiozidi 10 na kuwatumia wachezaji wasiozidi nane katika mchezo mmoja.