Bodi ya ligi yasogeza mbele mchezo wa Simba na Yanga

0
64

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imefanya mabadiliko katika mchezo Na.61 wa msimu wa 2020/2021 kati ya Young Africans SC na Simba SC uliokuwa uchezwe Oktoba 18,2020. Sasa utachezwa Novemba 7, 2020 saa 11:00 jioni kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Mabadiliko hayo yametokana na uwezekano mkubwa wa kuwepo kwa vikwazo katika usafiriwa kimataifa baada ya kukamilika kwa michezo ya kimataifa iliyo kwenye kalenda ya FIFA jambo ambalo linaweza kuathiri vikosi vya klabu hizo mbili.

Nchi nyingi bado zimeendelea kuweka masharti magumu katika taratibu za usafiri wa kimataifa tangu kuzuka kwa janga la virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19.

Send this to a friend