Bodi ya Wakandarasi yafuta makampuni 1766 kwa kukiuka sheria

0
23

Bodi ya Usajili wa Wakandarasi (CRB) imetangaza kuzifuta katika orodha yake jumla ya makapuni 1731 zinazomilikiwa na wazawa kutokana na kushindwa kukidhi vigezo vya kuweza kusajiliwa.

Bodi hiyo ambayo ni chombo cha serikali kilichoundwa kwa malengo ya kulinda maslahi ya makampuni hayo lakini pia kusimamia huduma zinazotolewa kwa wateja, imesema kuwa ufutwaji wa makampuni hayo umeanza rasmi Oktoba Mosi 2019.

Mbali na kampuni hizo, bodi hiyo pia imezifuta katika orodha yake jumla ya kampuni 35 za kigeni kutokana na sababu hiyo hiyo ya kutokidhi vigezo vya usajili.

Unaweza kupakua orodha ya kampuni hizo, bonyeza hapa

Send this to a friend