Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Patrobas Katambi amesema Serikali tayari imeunda bodi kwa ajili ya kufanya upembuzi ili kupata kima cha chini cha mshahara kwa sekta binafsi.
Ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuelezea maadhimisho ya wiki ya vijana itakayoanza kesho, ambapo amesema kazi hiyo ya upembuzi inatarajiwa kuanza Oktoba 07 mwaka huu.
“Tutarajie kuwa hivi karibuni tutakuwa tumepata tangazo maalum la kazi waliyoifanya, kwa sababu wameshirikisha wadau wa sekta husika, hii imelenga kutatua changamoto katika sekta tofauti za binafsi,” amesema Katambi.
Ameongeza, hili linafanyika kwa kuangalia kiwango kilichopo cha sasa na kipya kulingana na kiwango cha uchumi na uhalisia wa maisha, kima cha chini cha mshahara kinachoendana na uhalisia.”