Bolt kusitisha huduma ya usafiri kwa wateja binafsi

0
54

Kampuni ya Bolt imetangaza kusitisha huduma za usafiri wa magari kwa baadhi ya wateja wake kuanzia Agosti 17, 2022 huku huduma hiyo ikibaki kwa wateja wa kampuni na taasisi pekee.

Tamko hilo limeeleza kuwa uamuzi huo ni kutokana na mazungumzo na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu (LATRA) kuchukua muda mrefu kuhusu utaratibu wa utoaji huduma ambao Bolt imedai umekuwa ukiwasababishia hasara.

Mnamo Machi mwaka huu LATRA ilipandisha gharama za nauli, utaratibu ambao pia ulisababisha kampuni ya Uber kusimamisha shughuli za usafiri katika mwezi uliofuata wa Aprili.

Hata hivyo Bolt iliendelea kutoa huduma hizo huku akishirikiana na LATRA kutatua suala hilo.

Send this to a friend