Bolt yasitisha safari kati ya Nigeria na Afrika Kusini baada ya kufanyiwa mzaha mtandaoni

0
77

Kampuni ya huduma za usafiri mtandaoni, Bolt imechukua hatua ya kuzuia maombi ya safari kati ya Nigeria na Afrika Kusini kufuatia mzozo wa mzaha uliosambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Watumiaji wa mitandao hiyo wamekuwa wakiomba (request)safari za taxi katika nchi nyingine kisha kughairi kama mzaha, jambo lililowafanya madereva kupoteza muda na mafuta bila kupata abiria.

Madereva wamekuwa wahanga wa mchezo huo wa kijanja ambapo wamejikuta wakiwatafuta abiria ambao hawakuwa hata kwenye nchi hiyo.

Mzozo huu pia umesababisha ongezeko la bei za safari katika nchi hizo mbili, na kuwafanya baadhi ya watu kushindwa kumudu gharama za usafiri.

Send this to a friend