Bomoa bomoa nyingine yanukia Kimara

0
51

TANROAD imetoa siku 30 (kuanzia Julai 9) lwa wakazi Kimara kuondoa kuta, vibada, mashimo ya maji taka, nyumba zilizopo katika hifadhi ya barabara kuanzia eneo la Kimara Bucha hadi Kimara Resort ili kuruhusu shughuli za uboresha unaolenga kutatua changamoto za foleni.

Kaimu Meneja wa TANROADS Mkoa wa Dar es Salaam, Mhandisi Eliamini Tenga amesema kutokana na ongezeko la magari kumekuwa na msongamano mkubwa wa magari kuanzia Kimara Korogwe mpanga Ubungo hususani nyakati za jioni.

Kwa mujibu wa sheria Hifadhi ya Barabara ya Morogoro ina upana wa mita 90 kutoka katikati mwa barabara kila upande kuanzia Ubungo mpaka Kimara Stop Over.

Hii haitakuwa mara ya kwanza kwa wakazi wa Kimara kushuhudia bomoa bomoa ikiwakumba kwani itakumbukwa mwaka 2017 TANROADS iliendesha shughuli ya ubomoaji kupisha upanuzi wa barabara kutoka Kimara hadi Kiluvya.

Bomoa bomoa hiyo ilihusisha nyumba na mejengo 1,300 ambavyo yalijengwa kwenye hifadhi ya barabara  ambayo ni mita 121.5 toka katikati ya barabara.

Send this to a friend