Bondia Mtanzania aibuka bingwa Ujerumani

0
60

Bondia Mtanzania anayeishi nchini Sweden, Awadhi Tamim amemtwanga Bondia Shkelqim Ademaj wa Ujerumani kwa Technical Knock Out (TKO) katika pambano la raundi 10 lililofanyika Essen nchini Ujerumani usiku wa kuamkia Juni 12, 2022

Tamim ameshinda taji lililokuwa wazi la World Boxing Foundation (WBF International) baada ya mpinzani wake kushindwa kuendelea na pambano, na kueleza kuwa huo ni ushindi muhimu zaidi kwake.

Tamim alianza kwa kumlambisha sakafu Ademaj katika raundi ya sita lakini baadaye aliamka na kuruhusiwa kuendelea na pambano. Tamim aliongoza kwa pointi wakati wote wa pambano hilo hadi lilipovunjwa kutokana na Ademaj kushindwa kuendelea.

Hivi karibuni bondia huyo alikutana na kuzungumza na Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango alipokuwa ziarani nchini Sweden ambapo alimueleza juhudi zake katika kuitangaza Tanzania kupitia mchezo huo wa masumbwi.

Pia, alimuahidi kuiwakilisha vyema Tanzania katika pambano hilo la uzito wa juu lililofanyika Ujerumani.

Send this to a friend