Bosi Tigo aandika barua polisi kuomba pasi yake ya kusafiria

0
29

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tigo Tanzania anayeelekea kumaliza muda wake, Simon Karikari ameliandikia barua Jeshi la Polisi akiliomba kumrudishia pasi yake ya kusafiria. Katika barua yake ya Septemba 13, ameeleza kuwa nyaraka hizo zilichukuliwa tangu Februari 6 mwaka huu.

Karikari ameongeza kuwa kibali chake cha kuishi na kufanya kazi nchini Tanzania kinafikia ukomo Oktoba 1 mwaka huu. Amebainisha kwamba nyaraka zilizochukuliwa na ameiomba Polisi kumrejeshea ni pasi zake za kusafiria mbili, moja ya Uingereza na nyingine ya Ghana.

Bosi Tigo ‘akataa’ kuongeza mkataba

Mapema mwaka huu bosi huyo alieleza kwamba ataondoka kwenye kampuni hiyo kufuatia kuamua kutoongeza mkataba, pindi mkataba wake wa sasa utakapokwisha mwishoni mwa Septemba 2021.

Karikari anaondoka Tigo baada ya kuitumikia kwa miaka saba, ikiwemo mitano hapa nchini. Alianza kuitumikia Tigo Aprili 2016 akiongoza idara ya fedha (Chief Financial Officer), nafasi aliyoshika hadi Mei 2017 alipoteuliwa kuwa CEO.

Send this to a friend