BoT yaonya wanaotumia pesa kutengenezea maua

0
88

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imeonya matumizi mabaya ya pesa ikiwemo wale wanaotumia pesa hizo kutengeneza mashada na maua kwa ajili ya kuwatunuku wapendwa wao.

Akizungumza na Swahili Times, Meneja Msaidizi Kitengo cha Mawasiliano, Noves Moses amesema pesa inapotumika kufanya shughuli nyingine tofauti ni kukiuka utaratibu pamoja na kuipa gharama Serikali kutengeneza pesa mpya kutokana uchakavu wa pesa.

“Tuligundua pia maeneo mengi tu ya nchi utakuta noti zinatengenezewa mashada, zinatengenezewa maua, watu wengine wanatupa chini pesa au labda mtu anatoa burudani ile noti inachukuliwa inaenda kubandikwa sehemu yenye jasho, kichwani, kwenye paji la uso.

Kwahiyo matumizi ya namna hiyo ndiyo ambayo tunatolea ufafanuzi kwamba mnapofanya hivyo mnakiuka sheria, hizi ni pesa ambazo zinatumia gharama ambayo ingeweza kutumika kufanyia mambo mengine kwaajili ya ustawi wa jamii lakini sasa zinatumika kutengenezea noti mpya,” ameeleza.

Karia: Zawadi ya milioni 188 ya timu ya U15 itajengea miundombinu

Aidha, amesema elimu hiyo haikuwa imewafikia watu wengi, hivyo baada ya elimu inayoendelea kutolewa na BoT katika maeneo mbalimbali, hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa watakaovunja taratibu hizo.

Hata hivyo, BoT imewataka wananchi hususani wanawake kuepuka kukunja pesa au kuziweka kwenye maziwa na badala yake waweke kwenye pochi zitakazowawezesha kuweka noti ikiwa imenyooka.

Send this to a friend