BoT yataja orodha ya ‘Application’ za mikopo zisizokuwa na kibali

0
55

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imesema imebaini kuwepo kwa majukwaa na programu tumizi ‘Applications’ zinazojihusisha na utoaji wa mikopo kidijitali bila kuwa na leseni na idhini kutoka Benki Kuu.

BoT imetaja orodha ya programu hizo ambazo hazina kibali na kuutaka umma kutojishughulisha na program hizo, huku ikieleza kuwa inashirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuzifungia ili kuepusha umma kuzitumia.