Brazil: Waandamanaji wavamia Bunge na makazi ya Rais, wachana nyaraka

0
45

Maelfu ya waandamanaji wanaomuunga mkono aliyekuwa Rais wa Brazil, Jair Bolsonaro wamevamia makazi ya Rais, Bunge na Mahakama ya Juu katika mji mkuu, Brasília, Jumapili Januari 8, 2023, wengi wakitaka uingiliaji wa kijeshi ili kumwondoa Luiz Inácio Lula da Silva, kiongozi aliyechukua madaraka wiki iliyopita.

Waandamanaji hao waliokuwa wamevalia rangi za kitaifa ambazo ni kijani kibichi na manjano, waliingia katika majengo muhimu ya serikali huku wakivunja madirisha na samani pamoja na kurarua nyaraka kabla ya polisi wa kutuliza ghasia kuwaondoa ambapo takribani watu 400 wamekamatwa.

Aidha, takribani wanahabari watano wameshambuliwa wakati wa ghasia hizo na waandishi wengine wakiibiwa vifaa vyao kwa mujibu wa Chama cha Wanahabari wa Uchunguzi wa Brazil (ABRAJI).

Taarifa kutoka nchini humo zinaeleza kuwa kwasasa hali iko chini ya udhibiti katika eneo hilo.

Send this to a friend