BRELA: Hatujapokea malalamiko kuhusu Kampuni ya Kalynda

0
28

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) umesema haujapokea malalamiko rasmi kuhusiana na Kampuni ya Kalynda E Commerce Limited ambayo inadaiwa kukusanya fedha kutoka kwa wananchi kwa ahadi ya kupata faida ndani ya muda flani na kwamba walalamikaji wanapaswa kwenda mahakamani.

Ameyasema hayo Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Makampuni na Majina ya biashara, Meinrad Rweyemamu alipokuwa akifanyiwa mahojiano na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).

BRELA: Kalynda ilipewa leseni ya kuuza vifaa vya kielektroniki

Ameongeza kuwa kampuni hiyo ni halali kwa kuwa ilitimiza vigezo vya kusajiliwa na kwamba kuna taratibu za kufuata ili kufuta kampuni kwa kuwa kwa sasa bado inatuhumiwa.

Aidha, Rweyemamu amewashauri Watanzania kufanya utafiti kabla ya kuingia makubaliano na kampuni ikiwemo kuuliza kwa Wakala wa Usajili ili kupata uhakika wa usajili wa kampuni husika kwakuwa ni haki ya mwananchi.

Taarifa ya BRELA ilisema leseni ya kampuni hiyo ni kwa ajili ya uuzaji wa jumla wa vifaa vya kielektroniki na mawasiliano pamoja na ufanyaji wa biashara ya kiteknolojia ya kimataifa mtandaoni.

Send this to a friend