BRICS yaongeza wanachama wapya sita zikiwemo Ethiopia na Misri

0
32

Baada ya nchi 20 kuwasilisha maombi ya kutaka uanachama, viongozi wa kundi la mataifa ya BRICS yaani Brazil, Urusi, India, China na Afrika Kusini wamekubaliana kuyaalika mataifa sita kujiunga na BRICS baada ya majadiliano ya muda mrefu.

Katika mkutano huo unaofanyika nchini Afrika Kusini, ulioanza Agosti 22,2023 na kuhudhuriwa na viongozi wa mataifa mbalimbali akiwemo Rais wa Tanzania, Rais Samia Suluhu Hassan, viongozi hao wameridhia kuiongeza, Argentina, Misri, Ethiopia, Iran, Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu ambapo utekelezwaji wa uanachama huo utaanza Januari 2024.

“Kama nchi tano za BRICS, tumefikia makubaliano juu ya kanuni za mwongozo, viwango, vigezo, na taratibu za mchakato wa kupanua BRICS ambao umekuwa kwenye majadiliano kwa muda mrefu,” amesema Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa.

Balozi wa Marekani: Demokrasia ya Tanzania lazima ifanane na Tanzania

BRICS imesema hayo ni makubaliano ya awamu ya kwanza ya mchakato huo wa kupanua kundi hilo na awamu nyingine itafuata. BRICS imeeleza kuwa inathamini maslahi ya nchi nyingine katika kujenga uhusiano bora na kundi hilo.

Mnamo 2006, nchi nne ziliamua kujiunga pamoja kama kikundi cha BRIC na Afrika Kusini ilijiunga mwaka 2010 na hivyo kuuita BRICS. Kwa pamoja, nchi za BRICS zina idadi ya watu bilioni 3.24 na mapato yao ya kitaifa yanafikia $26 trilioni [quadrilioni 65.14] ambayo ni asilimia 26 ya uchumi wa dunia.

BRICS iliundwa kutafuta njia za kuleta mageuzi katika taasisi za fedha za kimataifa kama vile Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia ili kuwa na nguvu na kuwakilisha mataifa yanayoibukia kiuchumi.

Send this to a friend