Bugando kutafiti chanzo cha watu wengi Kanda ya Ziwa kuwa na tatizo la kusikia

0
44

Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando mkoani Mwanza inatarajia kuanza utafiti ili kubaini sababu za idadi kubwa ya watu wenye tatizo la kusikia katika Kanda ya Ziwa, hasa katika mikoa ya Shinyanga na Geita.

Akizungumza katika kilele cha Siku ya Usikivu Duniani, Mkurugenzi Mkuu wa hospitali hiyo, Dkt. Fabian Massaga amesema pamoja na kupungua kwa idadi ya watu wenye matatizo hayo bado tatizo ni kubwa ambapo mnamo 2020 watu 1,635 waligundulika, asilimia 49.06 wakiwa watu wazima na asilimia 50.94 wakiwa watoto.

Ameongeza kuwa mwaka 2021 watu 856 waligundulika kushindwa kusikia, ambapo asilimia 68.97 walikuwa watu wazima na asilimia 31.03 wakiwa watoto, huku mwaka 2022 idadi ya waliogundulika ilikuwa 970, asilimia 68.77 wakiwa watu wazima na asilimia 31.23 ni watoto.

Mtoto afariki akiombewa apone malaria

Vile vile, amesema hospitali ya Bugando hivi karibuni itakuwa na utaratibu wa zoezi la uchunguzi wa masikio ya watoto wachanga mara baada ya kuzaliwa ikiwa ni katika jitihada za kukabiliana na matatizo hayo katika hatua za awali.

Naye Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa, Dk Silas Wambura amesema Serikali pia inapambana kuanzisha huduma za masikio, pua na koo katika hospitali zote za Mwanza, hatua inayolenga kupambana na matatizo ya kusikia katika hatua za awali na kuleta huduma katibu na wagonjwa.

Send this to a friend