Bunge la Ghana lakatiwa umeme kwa kutolipa deni

0
40

Kampuni ya umeme ya Ghana (ECG) imekata kwa muda usambazaji wa umeme kwenye jengo la bunge siku ya Alhamisi baada ya bunge kushindwa kulipa deni lake la TZS bilioni 4.5.

Video iliyosambaa kwenye vyombo vya habari nchini humo imeonyesha wabunge wakipaza sauti katika ukumbi wa bunge wakiwa gizani baada ya umeme kuzimwa, wakiimba “dumsor, dumsor” yaani kukatika kwa umeme kwa lugha ya Twi.

APHFTA wagoma kutoa huduma kwa kitita kipya cha NHIF

Mkurugenzi wa ECG, William Boateng amesema kukata umeme kwenye jengo la bunge ilikuwa sehemu ya mkakati wa kawaida wa ECG kuhamasisha wateja wenye madeni kulipa.

“Walilipa [Bunge] cedi milioni 13 (TZS bilioni 2.5) na wakaahidi kulipa iliyobaki ndani ya wiki moja, hivyo wenzetu waliwaunganisha tena,” amesema Boateng.

Mbinu hii inakuja wakati sekta ya umeme ya nchi hiyo ikiwa inakabiliana na madeni mengi yasiyolipwa ambayo yamesababisha kuongezeka kwa kasi kwa kukatika kwa umeme huku kukiwa na mvutano kati ya wazalishaji wa umeme na serikali.

Send this to a friend