Bunge laahirisha kujadili muswada wa bima ya afya kwa wote

0
38

Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson ametangaza kuahirishwa kwa mjadala wa Muswada wa Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote kutokana na bunge pamoja na Serikali kuendelea na mashauriano juu ya mambo ambayo hayajaafikiwa.

Akizungumza leo Novemba 11, 2022 bungeni Dodoma Dkt. Tulia amesema bunge halitoutazama muswada huo uliosomwa kwa mara ya kwanza katika bunge lililopita na kupelekwa katika Kamati ya Kudumu ya Huduma ya Maendeleo ya Jamii ambao ulipaswa kuwasilishwa na Waziri wa Afya ili kujadiliwa leo bungeni hapo.

“Muswada huu utaletwa hapa bungeni tutakapokuwa tayari tumeshamaliza hayo mashauriano,” amesema Spika Tulia, ambapo leo muswada huo ulitarajiwa kusomwa kwa mara ya pili na ya tatu.

Aidha, amesema bunge linaendelea na mashauriano katika hoja kadhaa ambazo zimeibuliwa na wabunge, wadau mbalimbali waliojitokeza kwenye kamati na zingine Serikali inaendelea kuzitazama na kuangalia namna bora ya kuwahudumia wananchi kupitia bima za afya.

Send this to a friend