Bunge laazimia Serikali kununua ndege nyingine kuwahudumia viongozi

0
39

Bunge la Tanzania limeazia kuwa serikali ina haja ya kuona umuhimu wa kununua ndege mpya kwa ajili ya kuhudumia viongozi wakuu wa kitaifa.

Taarifa iliyotolewa bungeni leo Februari 13, 2024 na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Joseph Mhagama imeeleza kuwa azimio hilo limetokana na changamoto zinazokabili Wakala wa Ndege za Serikali katika kutoa huduma kwa wakati kwa viongozi wakuu pale wanapohitajika kwa wakati mmoja.

Kwa mujibu wa Mhagama, kamati yake imebaini kuwa kuna ndege tatu zinazotumiwa kwa ajili ya huduma za viongozi wa Serikali, ambapo moja inahudumia Rais wa Tanzania na nyingine mbili Fokker 50 na Fokker 28 zinawahudumia Makamu wa Rais, Rais wa Zanzibar, Waziri Mkuu, Makamu wa Kwanza na Wa Pili wa Rais wa Zanzibar, pamoja na viongozi wengine wa kitaifa hali inayopelekea utekelezaji wa jukumu hilo kuchelewa linapotokea safari za viongozi wote kwa wakati mmoja.

Kutokana na hali hiyo, Bunge limeazimia kwamba Serikali ione haja ya kufanya ununuzi wa ndege nyingine mpya ili kuboresha utoaji huduma za usafiri wa anga kwa viongozi wakuu wa kitaifa.

Send this to a friend