Bunge laiagiza Serikali kuharakisha ujenzi Bandari ya Bagamoyo

0
45

Bunge limeitaka Serikali kurahakisha ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo ili kuhakikisha uwepo wa mizigo ya kutosha itakayosafirishwa kupitia reli ya kisasa (SGR) kwenda mikoa mbalimbali na nchi jirani.

Azimio hilo limepitishwa leo bungeni jijini Dodoma baada ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma kuwasilisha taarifa yake ya ukaguzi kwa mwaka 2020/21 iliyolenga kulijulisha Bunge, iwapo uwekezaji wa mitaji ya umma una ufanisi na kwamba umezingatia taratibu, sheria na miongozo mujarabu ya biashara au vinginevyo.

Marubani waliogoma Kenya wapewa saa 24 kurejea kazini

Kamati imesema Serikali imetumia fedha nyingi kwenye mradi huo na kwamba “mradi huo wa uwekezaji utakapokamilika, SGR itakuwa na uwezo mkubwa wa kubeba mizigo, takribani tani 10,000 kwa safari. Mizigo mingi inatarajiwa kutoka Bandari ya Dar es Salaam ambayo haina uwezo wa kuingiza na kupakua kiasi hicho cha mzigo.”

Kutokana na kuwa kukosekana kwa mizigo ya kusafirisha kwa kadiri ya uwezo wa reli kutokana kutaathiri tija ya mitaji inayowekezwa kwenye bandari na SGR, bunge limeiagiza Serikali kuharakisha ujenzi wa bandari hiyo mpya.

Aidha, Serikali imeagizwa kusimamia kuongeza ufanisi wa Bandari ya Dar es Salaaam ikiwa ni pamoja na kuongeza Gati za kisasa katika Bandari ya Dar es Salaam lengo la yote haya ni kusaidia.

Send this to a friend