Bunge laipa Serikali hadi Juni 2024 kumaliza mgao wa umeme

0
53

Serikali imesema kufikia Machi mwaka huu mgao wa umeme unatarajiwa kumalizika baada ya kufanikiwa kufanya majaribio ya mtambo namba tisa katika Bwawa la Kufua umeme la Julius Nyerere (JNHPP).

Akijibu swali la Mbunge wa Lupembe, Edwin Swalle, Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga amesema majaribio ya mtambo huo uliofanyika Februari 15 umefanikiwa kwa kiasi kikubwa na ratiba ya kuuzindua mtambo huo ipo palepale pamoja na mtambo namba nane ambao utaanza kuzalisha umeme ifikapo Machi.

“Tunawashukuru sana waheshimiwa wabunge na Watanzania kwa uvumilivu na kuendelea kutuvumilia, tunataka kuwahakikishia kuwa ratiba ambayo tulisema ya uzinduzi wa mradi ipo kama ambavyo tulikuwa tumepanga,” amesema Kapinga.

Tume ya uchaguzi yatangaza uchaguzi wa madiwani kwenye Kata 23

Ameongeza kuwa kwa mara ya kwanza serikali ilitegemea mtambo namba tisa ungewashwa mwezi wa sita lakini kwa jitihada za Serikali na wakandarasi walifanikiwa kuharakisha zoezi hilo.

Hata hivyo, Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson ameipa muda Serikali hadi kufikia mwezi Juni ili kumaliza mgao wa umeme kwakuwa ndio muda uliopendekezwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Send this to a friend