Bunge lampongeza Rais Samia kwa kushinda tuzo ya Mjenzi Mahiri

0
52

Bunge la Tanzania limetoa azimio la kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwa miongoni mwa viongozi wenye ushawishi zaidi duniani, pamoja na kupokea tuzo ya mafanikio ya ujenzi wa miundombinu.

Katika mkutano wake wa saba, kikao cha 31, bunge limeazimia kumpongeza Rais Samia kwa kutambuliwa na kupewa tuzo kuu ya Mjenzi mahiri ya Babacar Ndiaye nchini Ghana kufuatia mafanikio makubwa ya Serikali ya Awamu ya sita katika Ujenzi wa Miundombinu nchini Tanzania.

Musukuma ataka wazee wapelekwe JKT

Aidha, Bunge limeazia kumpongeza Rais Samia kwa kutambuliwa kama miongoni mwa viongozi wenye ushawishi mkubwa Duniani, jambo linaloiletea sifa nzuri nchi ya Tanzania.

Pamoja na hayo, kumpa moyo Rais Samia kwa juhudi mbalimbali anazoendelea kuzichukua katika kuiletea nchi ya Tanzania maendeleo.

Send this to a friend