Bunge lataka serikali kuanzisha mamlaka ya kusimamia nyumba za kupanga

0
20

 

Bunge la Tanzania limependekeza kuanzishwa kwa Mamlaka ya kusimamia Sekta ya Nyumba Nchini (Real Estate Regulatory Authority – RERA) ambayo pamoja na majukumu mengine itasimamia upangishaji wa nyumba.

Hoja hiyo imetolewa bungeni na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Aridhi, Maliasili na Utalii, Ally Makoa wakati akiwasilisha taarifa ya mwaka ya shughuli za kamati kipindi C cha Januari 2021 hadi Februari 2022.

Makoa amelieleza bunge kwamba “kukosekana kwa mamlaka ya kusimamia sekta ya Nyumba kumepelekea kuwepo kwa utitiri wa madalali wa nyumba, uholela wa bei za kupanga na hata kuikosesha mapato serikali kwa kiasi kikubwa.”

“Bunge linashauri kwamba, Serikali iharakishe mchakato wa kuanzisha Mamlaka ya kusimamia Sekta ya Nyumba ili kuwepo na chombo madhubuti kinachosimamia sekta ya nyumba nchini,” ameongeza Makoa.

Send this to a friend