Burna Boy awaomba radhi mashabiki wake

0
44

Msanii wa muziki wa Nigeria, Damini Ogulu ‘Burna Boy’ ameomba radhi mashabiki zake kufuatia kuchelewa kwake kwenye tamasha lake la ‘Lagos Loves Damini’ usiku wa kuamkia Jumatatu huko Lagos nchini Nigeria.

Kwa mujibu wa mashabiki ambao wametoa malalamiko yao kwenye mitandao ya kijamii, wamedai tamasha hilo lilipangwa kuanza saa 12 jioni lakini halikuanza muda huo hadi ilipofika saa nne usiku, kisha iliwabidi kusubiri hadi saa 9 usiku muda ambao alipanda jukwaani.

Hata hivyo mwanamuziki huyo hakuomba msamaha kwa kitendo hicho, bali aliwaambia wanaomchukia kwamba ‘Mungu atawaadhibu’ hali iliyosababisha hasira kwa mashabiki ambao waliingia kwenye mitandao ya kijamii kueleza masikitiko yao dhidi yake.

Akijibu malalamiko hayo, Burna Boy kupitia ukurasa wake wa Twitter ameeleza kuwa muundo na miundombinu ya nchi haikuweza kukidhi mahitaji yake na kuwalaumu waandaji kwa kuchelewa kwake kupanda jukwaani, kisha kuwaomba radhi kwa kuwafanya wasubiri kwa muda mrefu na kuwashukuru kwa kustahimili dhoruba pamoja naye.

Send this to a friend