Burundi yafunga mipaka yake na Rwanda

0
44

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Burundi, Martin Niteretse, ametangaza kwamba serikali yake imefunga mipaka yake na Rwanda kuanzia Alhamisi, Januari 11, 2024.

Uamuzi huo unafuatia hotuba ya Rais wa Burundi, Evariste Ndayishimiye, ambaye alishutumu Rwanda kwa kufadhili kikundi cha waasi cha Red-Tabara, kilichofanya mashambulizi ya ardhini na kusababisha vifo vya watu 20 Desemba mwaka jana.

“Kwa sababu tumegundua tuna jirani mbaya, Paul Kagame, Rais wa Rwanda, tumesitisha uhusiano naye hadi atakapobadilika,” alisema Niteretse na kuongeza kuwa “tumefunga mipaka leo, yeyote anayesafiri hatavuka.”

Waasi wa Burundi wa Red Tabara walidai kuhusika na shambulio hilo lakini walisema kuwa waliwaua wanajeshi tisa tu na afisa mmoja wa polisi.

Serikali ya Rwanda ilikanusha tuhuma hizo huku ikitoa taarifa kwamba haihusiki kwa njia yoyote na kundi linaloishambulia Burundi.

Send this to a friend