Bwawa la Kariba lasitisha kuzalisha umeme wa Zimbabwe kutokana na ukame

0
57

Mamlaka ya Mto Zambezi (ZRA) imeagiza kusimamishwa kwa uzalishaji wa umeme katika Bwawa la Kariba ambalo husambaza umeme kwa mamlaka ya umeme Zambabwe, hadi Januari, kutokana na upungufu wa maji.

Ukame umepelekea maji katika bwawa kupungua ambapo maji yaliyopo katika bwawa hilo kwa sasa ni asilimia 4.6% ya uwezo wake, ikiwa ni chini ya kiwango kinachotakiwa kuendesha uzalishaji wa umeme, ZRA ambayo inasimamia bwawa hilo kwa niaba ya Zambia na Zimbabwe imesema.

Mamlaka hiyo imesema haikuwa na njia nyingine zaidi ya kuchukua hatua hiyo, ambapo Januari 2023 itafanya mapitio mengine kuona hali itakavyokuwa.

Zimbabwe huzalisha megawati 1,050 za umeme kutoka katika Bwawa la Kariba ambalo uwezo wake ni kuzalisha megawati 2,100.