CAF yaipiga faini Kenya milioni 127 baada ya mechi na Morocco

0
139

Shirikisho la Soka Kenya (FKF) limepigwa faini ya Dola za Kimarekani 50,000 [TZS milioni 127.8] kwa makosa ya kiusalama katika mechi dhidi ya Morocco iliyofanyika Uwanja wa Moi, Kasarani.

Aidha, Bodi ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) imetishia kuhamishia mechi za timu ya Kenya nchini Uganda au Tanzania iwapo makosa hayo yataendelea.

Mbali na onyo hilo, CAF pia imeishauri Kenya kuongeza ulinzi kwa kuweka walinzi wa kutosha kuzunguka eneo la uwanja na kuhakikisha barabara zinafungwa siku za mechi.

Kenya, Uganda na Tanzania ni wenyeji wa Michuano ya Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN- 2024).

Send this to a friend