CAF yaufungia Uwanja wa Benjamin Mkapa

0
3

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeufungia kwa muda Uwanja wa Benjamin Mkapa uliopo Dar es Salaam kutokana na eneo la kuchezea (pitch) kuendelea kupungua ubora wake.

CAF imeielekeza Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kutuma jina la uwanja mbadala utakaotumiwa na Simba kwenye mchezo wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Masry kufikia Machi 14, 2025.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Machi 12, 2025 na Afisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Cliford Mario Ndimbo, CAF imesema eneo hilo liboreshwe haraka kufikia viwango vinavyotakiwa ili kuepuka uwanja huo kufungiwa kwa muda mrefu.

Aidha, CAF imesema itafanya ukaguzi wa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Machi 20, 2025 ili kuona maboresho yaliyofanyika kabla ya kuamua kuuruhusu utumike au kuendelea kuufungia.

Send this to a friend