CAG aipongeza TANROAD ujenzi wa Uwanja wa Ndege Msalato

0
4

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichere amepongeza kasi ya ujenzi wa uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato wenye ukubwa wa hekta 4,500 ( hekari 11000).

CAG Kichere ametoa pongezi hizo wakati alipofanya ziara ya kikazi ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa uwanja cha ndege wa Msalato Jijini Dodoma.

Katika ziara hiyo ambayo aliambatana na maafisa kutoka ofisi ya CAG amempongeza Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara Tanzania-TANROADS Mhandisi Mohamed Besta pamoja na Wakandarasi wanaotekeleza ujenzi wa uwanja huo wa Msalato ambapo amesema kuwa muda mwingi husoma ripoti za miradi akiwa ofisini pasipo kujionea mambo makubwa yanayofanywa na serikali.

“Katika ripoti zetu za ukaguzi tunasoma lakini ni vyema kuja kama hivi kujionea ni kitu gani kinachoendelea eneo la mradi, kwahiyo tumeona nini kimetokea” Amekaririwa CAG Kichere

Kichere amehimiza wakandarasi wa mradi huo kufanya kazi usiku na mchana ili kukanilisha mradi huo kwa wakati unaotakiwa ambapo pia ametoa wito kwa wananchi kutovamia maeneo hayo ya uwanja kwani ni alama ya mkoa wa Dodoma na Taifa kwa ujumla wake.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Mhandisi Mohamed Besta amesema uwanja huo utakamilika rasmi mwezi Novemba 2025 na kuanza kutumika ifikapo Julai 2025.

 

 

Send this to a friend