CAG Zanzibar aliomba radhi Baraza la Wawakilishi kwa kutoa kauli ya ‘kulibeza’

0
23

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Zanzibar, Dkt. Othman Ali ameliomba radhi Baraza la Wawakilishi Zanzibar kufuatia kauli yake aliyoitoa ambayo ilionekana kuwabeza wajumbe wa baraza hilo.

Hivi karibuni wakati akiwakilisha ripoti ya CAG mwaka 2022/23, Dkt. Othman alinukuliwa akisema kamati za ukaguzi za baraza hilo hazina uwezo wa kufanya kazi zao kwa ufanisi.

Kufuatia kauli hiyo, hoja mbalimbali ziliibuliwa ambapo wajumbe watatu wa baraza hilo walitaka mwongozo wa Spika kuhusu kauli ya CAG na kumtaka aombe radhi juu ya kauli yake.

Akitoa mwongozo, Spika wa Baraza la Wawakilishi, Zubeir Maulid amesema Dkt. Othman amesamehewa baada ya kufika ofisini kwake na kukiri kuwa maneno yake yameleta tafsiri mbaya na hivyo kuliomba radhi baraza hilo.

Balozi aliyewafananisha Waafrika na nyani arudishwa kwao

“Kutokana na kitendo hicho cha uungwana alichokifanya CAG, Dkt. Othman Abbas Ali cha kufika Ofisi ya Spika na kutoa maelezo ya kuomba radhi kwa baraza, imenifanya nikubaliane na CAG kuhusu kuomba radhi kwake na kumeniridhisha kutoa maelezo na mwongozo wangu kwa baraza,” amesema.

Ameongeza kuwa “Naomba kutoa mwongozo wangu huu na kusitisha mjadala wowote juu ya swali hili ndani na nje ya Baraza la Wawakili, mjadala huu umefungwa, itoshe tu kwa baraza hili kupokea ombi la CAG la kuomba radhi na waheshimiwa wajumbe mlichukue na kulipokea hivyo kama lilivyo.”

Send this to a friend