Canada kuomba msaada wa Mfalme Charles dhidi ya Trump

0
3

Waziri Mkuu wa Canada, Justin Trudeau amesema atazungumza na Mfalme Charles III wa Uingereza na kipaumbele chake kitakuwa kulinda uhuru wa nchi yake, baada ya Rais Donald Trump kupendekeza kuifanya Canada kuwa jimbo la 51 la Marekani.

Trudeau amesema hakuna jambo muhimu zaidi kwa raia wake kuliko kusimamia uhuru wa watu wake na kujitegemea.

Trump amependekeza mara kadhaa kwamba Canada ingekuwa katika hali bora zaidi ikiwa ingekubali kuwa jimbo la 51 la Marekani.

Mwezi uliopita, Trudeau alionya kuwa tishio la Trump la mara kwa mara kuhusu kuichukua Canada ni suala la kweli, na linahusiana na utajiri wa rasilimali asili za nchi hiyo.

Send this to a friend